Staa asiyekaukiwa na vituko, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’.
Hamida Hassan
Staa asiyekaukiwa na vituko, Lulu Semagongo ‘Anti Lulu’
ameonekana kulazimisha penzi kwa mwanamuziki Koffi Olomide kutokana na
maelezo yake kwamba anampenda na atahakikisha anampata.
Akizungumza na Ijumaa baada ya Koffi kutua nchini kwa ajili ya shoo
aliyoifanya Ukumbi wa Escape One jijini Dar, Anti Lulu alisema anampenda
sana mwanaume huyo, amekuwa akifikiria jinsi ya kujisogeza kwake lakini
anashindwa.
“Unajua nampenda sana Koffi, siyo kimuziki tu bali na kimapenzi.
Niliwahi kumsikia akisema anapenda wanawake waliofungashia sasa
nikiunganishwa naye unadhani atapindua kwangu. Yaani silali kwa sababu
ya penzi lake,” alisema Lulu.
0 comments:
Post a Comment