KATAZO! Nyota
wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando (pichani) amezuiwa kuingia
kanisani na ndugu zake wa damu kufuatia kile walichokiita ni kuchoshwa
na manyanyaso na kwamba endapo akienda kinyume na maagizo hayo
watachukua walichokitaja kuwa ni uamuzi mgumu, Amani linatumbua jipu!
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku nyingi
nduguze wamekuwa wakimtaka Rose kuachana na Ukristo, lakini amekuwa
‘ngangali’ kwa kuwa anafurahia huduma anayoitoa.
Hata hivyo, Rose anadaiwa kuwa na
msimamo wa kutokubaliana na ndugu hao lakini hivi karibuni alinyoosha
mikono kwa kutii amri kwamba, ndugu zake hawataki wamuone akiingia
kanisani.
“Kulikuwa na kikao kizito sana. Rose
alitakiwa afanye uamuzi mgumu kwani maneno makali ambayo amekuwa
akizushiwa kwamba tapeli, mara anabwia unga, si tu kwamba yanamuumiza
peke yake, hata ndugu hao. Ndiyo maana wameamua kumzuia kwa nguvu zao
zote kwenda kanisani,” kilisema chanzo kimoja.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta staa huyo
kwa njia ya simu ili kujiridhisha kwa kina na madai hayo ambapo kwa
sauti ya juu, alisema:
“Jamani! Unajua mimi naumwa! Nadhani
tuliwasiliana siku za nyuma (anamkumbusha mwandishi). Kwa hiyo tangu
siku zile bado hali yangu kiafya haijakaa sawa na ndiyo maana sijaenda
kanisani.
“Ni kweli kuna msuguano wa aina hiyo na
ndugu zangu. Si unajua hawajawahi kupendezwa na uamuzi wangu wa kuhama
Uislamu. Lakini mara zote nimekuwa nikiwaambia hakuna wa kuniondoa
kwenye Ukristo maana najua huyu Yesu alikonitoa.
“Kuna kaka yangu huyo ndiyo amekomaa
kunikataza. Nilimwambia mchungaji wangu (hakumtaja jina), akamfuata
lakini kaka akampiga mkwara mzito, yaani we acha tu.”
0 comments:
Post a Comment