Mashoga hao wakiwa mikononi mwa polisi,
picha ndogo(kushoto) ni mteja wao aliyedaiwa kuuawa.
Mashoga hao (pichani) Edwin Faulkner (kushoto) mwenye umri wa miaka 33 na Juan Carlos Martinez-Herrera ( 35) watayamalizia maisha yao gerezani.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Bonnie Wittner katika mahakama hiyo jana. Watu hao walimkaba kwa kumziba pumzi na kumwibia mteja wao huyo, John Laubach (57) Machi 2, 2012.
“Alikuwa mteja wangu, tulikuwa tunakwenda kwake kila mara ambako alikuwa ananilipa kwa kufanya naye ngono,” alikiri Martinez-Herrera katika mahakama hiyo.
Wawili hao walimwibia Laubach vito mbalimbali na vitu vingine vya thamani kabla ya kutorokea Jimbo la Miami.
Martinez-Herrera, ambaye alikuwa amevaa nguo za kiume wakati alipokamatwa, alitokea mahakamani akiwa na nywele ndefu na akizungumza kwa sauti ya kike.
0 comments:
Post a Comment