MREMBO Faiza Ally, ambaye amejizolea umaarufu baada ya
kutinga ukumbini akiwa amevaa ‘Pampers’ siku ya kuzaliwa
kwake, amefunguka kuwa kivazi kingine akachokivaa Desemba 19, Fukwe za
Coco Aqua kitawapa presha watu wengi kutokana na kuwa gumzo zaidi.
Akizungumza na kona ya Bongo Movies, Faiza ambaye ni mzazi mwenzake
na Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi alisema kuwa siku hiyo pia
itakuwa siku yake ya kuzaliwa hivyo kivazi atakachokivaa hakijawahi
kuvaliwa nchini.
“Pampers iliwashangaza watu lakini kwa kweli kivazi nitakachotinga safari hii hakijawahi kuvaliwa ulimwenguni kabisa.
Nitakuwa nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kutakuwa na
kiingilio, fedha itakayopatikana nitawasaidia watoto yatima,” alisema
Faiza.
0 comments:
Post a Comment