KATIKA
kipindi chote cha mwaka 2015, mastaa mbalimbali kunako Bongo Movies
wamejikuta wakiingia kwenye bifu na kufikia hatua ya kutoleana maneno
mazito huku wengine wakidiriki kuzichapa hadharani pasipo sababu za
msingi.
Kona ya Bongo Movie ilifanya tafiti na
kupata orodha fupi ya baadhi ya wasanii hao wa Bongo Movie waliokuwa
marafiki na kuishia kuwa kwenye bifu.
WEMA NA AUNT
Katika hali isiyo ya kawaida mashosti
wawili, changu chako, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel waliingia kwenye bifu
zito Mei, mwaka huu baada ya Aunt kuifanyia ‘promo’ Zari All White Party
iliyoandaliwa na Zarinah Hassan ‘Zari’ kwa kushirikiana na mwandani
wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Bifu hilo linasemekana lilianzishwa na Wema aliyekuwa mpenzi wa Diamond na Aunt kufanya hivyo ikaonekana kama amemsaliti.
Hamisa Mobet
Kama haitoshi bifu hilo lilizidi
kuchukua sura mpya hata baada ya kupatanishwa na watu wao wa karibu,
Wema hakuhudhuria kwenye arobaini ya mtoto wa Aunt (Cookie) na Aunt
hakualikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Wema.
LULU NA HAMISA
Staa wa filamu asiyechuja tangu utotoni,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ naye aliingia kwenye bifu na mwanamitindo
maarufu Bongo, Hamisa Mobeto baada ya kumtuhumu kuwa amemchukulia
mwanaume aliyezaa naye na kusababisha mwanaye kutopata matunzo
yanayostahili kutoka kwa baba yake.
BATULI NA WEMA
Katika kipindi cha kampeni (Oktoba),
Wema na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ waliibua urafiki baada ya mwanadada huyo
nyumba yake kuungua moto na kuhamishia makazi kwa Wema.
Huku wakionekana kupendana kama mapacha
kwa kuvaa sare na kuongozana kila kona, baada ya muda urafiki wao
uliingia doa hata kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Wema, Batuli
hakuhudhuria na mpaka sasa hakuna aliyetaka kufungukia bifu lao
lilisababishwa na nini.
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper
aliingia kwenye bifu na msanii mwenzake, Aunt Ezekiel katika kipindi cha
kampeni (Oktoba), ambapo wote walikuwa mashabiki wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na baada ya muda Aunt akahamia Chama
Cha Mapinduzi (CCM) ndipo Wolper akamshukia mwenziye kwa madai kuwa
kilichompeleka ni tamaofauti zao.a ya pesa na kuanza kutupiana vijembe
japo baada ya uchaguzi wameonekana kumaliza t
Wasanii hao waliingia kwenye timbwili la
aina yake katika kipindi cha kampeni ambapo awali Musa ‘Kitale’ alikuwa
mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Jimmy ‘Mafufu’
lakini baada ya muda Kitale alihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndipo
mwenzake akamchana kwa kitendo hicho na kuanza kupakana mitandaoni na
kutishiana kupigana huku bifu lao likipozwa na mashabiki.
Mastaa hawa waliokuwa mashosti wakubwa
ambao bifu lao ni la kitambo na mpaka mwaka unakatika limeshindwa
kuchukua sura mpya kwa kile kinachodaiwa kuwa Kajala alimchukua Kigogo
wa Wema anayefahamika kwa jina la CK.
Siku chache zilizopita wawili hao
walitibuana tena kwenye shoo ya Skylight Band iliyofanyika Fukwe za
Escape One, Mikocheni jijini Dar baada ya kila mmoja kumuonesha mwenziye
ufahari wa kutunza pesa jukwaani na Kajala kuibuka kidedea ndipo Wema
akiwa na timu yake akachukia na kumshambulia Kajala.
Wasanii hawa waliingia kwenye bifu
kipindi cha kampeni kwa kutupiana vijembe baada ya Chuchu Hans aliyekuwa
Chadema na Wolper kudumu siku chache tu na kuhamia CCM.
Wolper alitumia mitandao ya kijamii kwa
kumchana Chuchu kuwa ni msaliti, hata hivyo baada ya uchaguzi kuisha
walimaliza tofauti zao.
0 comments:
Post a Comment