Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’.
Richard BukosPenzi la dhati halifi! Kwa mara ya kwanza tangu
ndoa yake ivunjike miaka kadhaa iliyopita, the big boss wa Mashauzi
Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ amenaswa akioneshana mahaba niue
hadharani na zilipendwa wake, Jumanne Islam ‘Tevez’.
Tukio hilo lililopigwa chabo na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi
iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo
Kundi la Mashauzi Classic lilikuwa likizindua wimbo wake mpya uliokwenda
kwa jina la Jiamini.
Katika shughuli hiyo, Tevez aliwasili ukumbini hapo na kumkuta Isha
akiwa amepozi kona ndipo mdada huyo, akainuka na kwenda ‘kumchumu’
mumewe huyo wa zamani.
Wakati wakifanya yao, paparazi wetu alikuwa akiwafuatilia kwa umakini
sambamba na kuwapiga picha za mnato lakini Isha alipomshtukia, aligeuka
mbogo na kumchimbia mkwara:
“Jamani hebu tuachieni umbeya wenu huyu ana mtu wake na mimi nina mtu wangu hamtaki hata watu wasisalimiane jamaniii…”
Kwa upande wa Teves alisema hawezi kukumtupa Isha kwani wametoka mbali.
www.globalpublishers.co.tz
0 comments:
Post a Comment