Ayaaaaaaa!!! SAA 5 BAADA YA KOMBA KUZIKWA..WASANII WA BONGO MOVIE WAFANYA BONGE LA PARTY

Mchekeshaji Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ akiwakaribishwa wageni. 
ZIKIWA zimepita saa takriban sita tangu kuzikwa kwa msanii mahiri wa nyimbo za Kwaya, Kapteni John Komba, anayetajwa kuwa karibu zaidi na wasanii wa fani zote, Mchekeshaji Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ alifanya bonge la pati la kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ndani ya Hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya Jiji la Mwanza, usiku wa Jumanne iliyopita.

Katika pati hiyo ambayo waalikwa walikula na kunywa, mke wa mchekeshaji huyo aitwaye Zawadi ndiye alikuwa kivutio kwani watu wengi hawakutegemea kama Steve ameoa ‘kifaa’.
“Dah, hapa Steve ndiyo kamaliza mchezo kabisa, huwezi kuamini kama anaweza kuwa na mke mzuri namna hii, hapa amewapiga bao mastaa wenzake,” alisikika akisema muigizaji mmoja wa kike anayefanya kazi jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Suzzy.


Hata hivyo, katika sherehe hiyo kulikuwa na idadi kubwa ya wageni waliojitokeza wakiwemo mastaa kama vile Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Rich’ na wengineo ambao walikuwa marafiki wa marehemu Kapteni Komba.
Steve Nyerere akiwa na mke wake. 
Ijumaa lilifanya jitihada za kuongea na Steve ili kujua sababu za kufanya pati hiyo wakati msiba wa Kapteni Komba ukiwa bado ‘mbichi’ bila mafanikio lakini rafiki yake aliyedai si msemaji wa msanii huyo alisem walikuwa jijini Mwanza kikazi hivyo hawakuweza kuhudhuria mazishi ya Komba ndiyo maana Steve aliamua kufanya kitu katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment