Mastaa walioongoza kwa bifu 2015



wemanaauntKATIKA kipindi chote cha mwaka 2015, mastaa mbalimbali kunako Bongo Movies wamejikuta wakiingia kwenye bifu na kufikia hatua ya kutoleana maneno mazito huku wengine wakidiriki kuzichapa hadharani pasipo sababu za msingi.

Kona ya Bongo Movie ilifanya tafiti na kupata orodha fupi ya baadhi ya wasanii hao wa Bongo Movie waliokuwa marafiki na kuishia kuwa kwenye bifu.

WEMA NA AUNT
Katika hali isiyo ya kawaida mashosti wawili, changu chako, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel waliingia kwenye bifu zito Mei, mwaka huu baada ya Aunt kuifanyia ‘promo’ Zari All White Party iliyoandaliwa na Zarinah Hassan ‘Zari’ kwa kushirikiana na mwandani wake, Nasibu Abdul  ‘Diamond’.
Bifu hilo linasemekana lilianzishwa na Wema aliyekuwa mpenzi wa Diamond na Aunt kufanya hivyo ikaonekana kama amemsaliti.
hamisaHamisa Mobet
Kama haitoshi bifu hilo lilizidi kuchukua sura mpya hata baada ya kupatanishwa na watu wao wa karibu, Wema hakuhudhuria kwenye arobaini ya mtoto wa Aunt (Cookie) na Aunt hakualikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Wema.

LULU NA HAMISA
Staa wa filamu asiyechuja tangu utotoni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ naye aliingia kwenye bifu na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto baada ya kumtuhumu kuwa amemchukulia mwanaume aliyezaa naye na kusababisha mwanaye kutopata matunzo yanayostahili kutoka kwa baba yake.
Lulumichael.jpgElizabeth Michael ‘Lulu’.

BATULI NA WEMA
Katika kipindi cha kampeni (Oktoba), Wema na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ waliibua urafiki baada ya mwanadada huyo nyumba yake kuungua moto na kuhamishia makazi kwa Wema.

Huku wakionekana kupendana kama mapacha kwa kuvaa sare na kuongozana kila kona, baada ya muda urafiki wao uliingia doa hata kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Wema, Batuli hakuhudhuria na mpaka sasa hakuna aliyetaka kufungukia bifu lao lilisababishwa na nini.
WOLPER-GWANDA.jpgAUNT NA WOLPER
Staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper aliingia kwenye bifu na msanii mwenzake, Aunt Ezekiel katika kipindi cha kampeni (Oktoba), ambapo wote walikuwa mashabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na baada ya muda Aunt akahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndipo Wolper akamshukia mwenziye kwa madai kuwa kilichompeleka ni tamaofauti zao.a ya pesa na kuanza kutupiana vijembe japo baada ya uchaguzi wameonekana kumaliza t

jimmyymafufucut.jpgJIMMY MAFUFU NA KITALE
Wasanii hao waliingia kwenye timbwili la aina yake katika kipindi cha kampeni ambapo awali Musa ‘Kitale’ alikuwa mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Jimmy ‘Mafufu’ lakini baada ya muda Kitale alihamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndipo mwenzake akamchana kwa kitendo hicho na kuanza kupakana mitandaoni na kutishiana kupigana huku bifu lao likipozwa na mashabiki.

wema, kajalaKAJALA NA WEMA
Mastaa hawa waliokuwa mashosti wakubwa ambao bifu lao ni la kitambo na mpaka mwaka unakatika limeshindwa kuchukua sura mpya kwa kile kinachodaiwa kuwa Kajala alimchukua Kigogo wa Wema anayefahamika kwa jina la CK.
Siku chache zilizopita wawili hao walitibuana tena kwenye shoo ya Skylight Band iliyofanyika Fukwe za Escape One, Mikocheni jijini Dar baada ya kila mmoja kumuonesha mwenziye ufahari wa kutunza pesa jukwaani na Kajala kuibuka kidedea ndipo Wema akiwa na timu yake akachukia na kumshambulia Kajala.

chuchu.jpgCHUCHU NA WOLPER
Wasanii hawa waliingia kwenye bifu kipindi cha kampeni kwa kutupiana vijembe baada ya Chuchu Hans aliyekuwa Chadema na Wolper kudumu siku chache tu na kuhamia CCM.

Wolper alitumia mitandao ya kijamii kwa kumchana Chuchu kuwa ni msaliti, hata hivyo baada ya uchaguzi kuisha walimaliza tofauti zao.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment